Thursday 7 November 2013
Tanzania music recording studio, Blue Sky Records Tanzania, Kutoa free promo kwa wasanii chipukizi
Posted on 13:12 by Unknown
Blue Sky Records Tanzania, Kutoa free promo kwa wasanii chipukizi , Tanzania music recording studio
Na Magendela Hamisi
MTAYARISHAJI chipukizi wa muziki wa kizazi kipya katika studio ya Blue Sky Records Tanzania, Gideon Wambwe ‘Dat Dream’ amejigamba kuanza kuteka soko la tasnia hiyo baada ya nyimbo zilizotengenezwa kwake kuanza kutamba.
Akizungumza jana na Jambo Leo, Dar es Salaam mtozi huyo alisema licha ya kuanza kurekodi nyimbo kwa kipindi kifupi na kuzipeleka katika vituo vya redio zimeanza kushika chati.
Alitaja nyimbo hizo kuwa ni Upendo wa Dhati, iliyoimbwa na Nilsam Hussein ‘Nilsam’ na I Saw You ya msanii wa kike anayeitwa Suzan Kabela ‘Mutes The Matron’ zilizo kwenye mahadhi ya Bongo Fleva.
Alizitaja nyimbo nyingine alizotengeneza za mahadhi ya Injili ni Yesu Tangaulia na Mimi Najua za msanii anayeitwa Veronica Victor ambazo nazo kwa sasa zinafanya vema katika vituo vya redio nchini.
Dat Dream alisema kuwa anaamini baada ya mwaka huu atakuwa mbali katika kuibua vipaji vya wasanii chipukizi ambao wanarekodiwa nyimbo zao katika studio kwa gharama nafuu.
Wakati huo huo, Meneja Masoko wa Studio hiyo, Felix Maganga ‘MG’ alisema nguvu waliyoanza nayo si ya soda, malengo yao ni kufanya kazi na wasanii wachanga na wakubwa ili kufikia kiwango cha kimataifa.
“Tunaamini kuwa tumeanza vema katika kazi ya kutayarisha muziki kwani tayari baadhi ya kazi zimeanza kusikika katika media na kupokelewa vema na wadau, tunaamini tutafika tunapopataka,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment